Tume kuundwa kufatilia miradi ya maji jimbo la Bunda
29 November 2023, 8:08 am
Naibu Katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameagiza kuundwa kwa tume maalum ya kufuatilia miradi yote ya maji jimbo la Bunda ambayo inaonekana kukamilika wakati huo hakuna huduma yoyote ya maji.
Na Thomas Masalu

Mhandisi Mwajuma ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakazi ya kijiji cha Mugeta na Mihingo kufatia ziara aliyoifanya ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji ambayo serikali imewekeza fedha.
Katika ziara hiyo Naibu katibu mkuu ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo ambapo amesema yaliyopita yamepita hivyo wakazi wategemee mabadiliko kupitia ziara hiyo.
Naye mbunge wa jimbo la Bunda Boniphace Getere amesema wananchi hawana uadui na serikali bali wanachotaka ni kuona miradi ina kamilika na maji yatoke.
Ziara ya Naibu Katibu Mkuu wizara ya maji imefanyika katika Kata 7 ambazo ni Hunyari, Mugeta, Mihingo, Salama, Nyamuswa na Nyamaguta.