Ukosefu wa maji, upungufu wa mabweni tatizo chuo cha Kisangwa Bunda
18 November 2023, 8:48 pm
Imeelezwa kuwa ukosefu wa maji safi na salama, upungufu wa mabweni Bado ni changamoto chuo Cha Maendeleo ya wananchi kisangwa FDC.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa ukosefu wa maji safi na salama, upungufu wa mabweni Bado ni changamoto chuo Cha Maendeleo ya wananchi kisangwa FDC.
Hayo yamebainishwa mbele ya mgeni rasmi kupitia risala ya wahitimu na taarifa ya mkuu wa chuo hicho katika mahafali ya 37 ya chuo yaliyofanyika 17 Nov 2023.
Kupitia risala ya wahitimu wameiomba serikali kuwapelekea huduma ya maji tililika ya bomba chuoni kutokana idadi ya wanachuo kuongezeka kila mwaka ambapo mwaka huu chuo kina jumla wanafunzi wapatao 367 ukilinganisha na wanafunzi 355 kwa mwaka 2022.
Wanafunzi hao wamesema kipindi Cha kiangazi hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji ambayo pia siyo salama kwa kuwa yanatumiwa pia na mifugo.
Naye mkuu wa chuo hicho Mwl Edmundi Nzowa akisoma taarifa ya chuo mbele ya mgeni rasmi amesema changamoto ya maji na upungufu wa mabweni bado ni tatizo kwao kutokana na kuongezeka Kwa Kwa idadi ya wanafunzi kila mwaka ambapo Kwa Sasa wanalazimika kutumia baadhi ya vyumba vya madarasa kuwa mabweni.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda Ndugu Emmanuel Mkongo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo amesema changamoto ziliainishwa kupitia risala ya wanafunzi na taarifa ya mkuu wa chuo amezichukua na atazifikisha Kwa Mhe mkuu wa wilaya ili kuona namna ya kuzitatua.
Aidha Mkongo amewataka wanafunzi wanaohitimu kutumia fursa zilizopo hasa za mikopo ya halmashauri isiyo na riba ambayo itasaidia kuendeleza fani zao ili kujiongezea kipato badala ya kusubili ajira.