Wanafunzi 4953 kidato cha nne Bunda kuanza mtihani Nov 13
12 November 2023, 7:43 pm
Wanafunzi wapatao 4953 kidato cha nne wanatarajia kuanza mtihani wa kuhitimu kidato cha nne wilayani Bunda kati yao wasichana ni 2470 na wavulana 2483.
Na Adelinus Banenwa
Wanafunzi wapatao 4953 kidato cha nne wanatarajia kuanza mtihani wa kuhitimu kidato cha nne wilayani Bunda kati yao wasichana ni 2470 na wavulana 2483.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano wakati akifanya mahojiano na radio Mazingira Fm.
Mhe Naano amesema hadi sasa maadandalizi ya mitihani hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na semina elekezi kwa wasimamizi wa mitihani na usambazaji wa mitihani katika maeneo husika miongoni.
Aidha Mhe Dkt Naano ameonya kwa wazazi na walezi, walimu pamoja na wanafunzi wenyewe juu ya kujihusisha na aina yoyote ya wizi na udanganyifu katika mitihani hii kuwa hwatosita kuwachukulia hatua watakaobainika.
Ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa baraza la mitihani Tanzania NECTA mitihani ya kuhitimu kidato cha nne itaanza tarehe 13 November 2023, na utatamatika tarehe 30 november 2023.