Ujenzi wa Sekondari Bunda Mjini wafikia 85%
9 November 2023, 8:05 am
Ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bunda Mjini unagharimu shilingi 584 mil chini ya mradi wa SEQUIP yafikia asilimia 85.
Na Adelinus Banenwa
Ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bunda Mjini unagharimu shilingi 584 mil chini ya mradi wa SEQUIP yafikia asilimia 85.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda Mhe Emmanuel Mkongo wakati akizungumza na Radio Mazingira FM ofisini kwake
Ujenzi huo wa shule ya Sekondari ya Bunda mjini unajibu changamoto ya muda mrefu Kwa wakazi wa kata hiyo ambao hawakuwa na shule ya Msingi, Wala Sekondari wa kituo Cha huduma za afya Cha serikali.
Mkongo ameiambia Mazingira Fm kuwa ujenzi wa shule hiyo unajumuisha vyumba nane vya madarasa, maabala 3, maktaba, chumba Cha tehama, jengo la utawala, tenki la maji la ardhini pamoja na kichomea taka.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema ujenzi wa shule hiyo utakamilika mapema ili January 2024 iweze kupokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza.
Ufafanuzi huu wa Mkurugenzi umekuja baada ya wakazi wa Bunda mjini kuishukuru serikali Kwa kuwakumbuka Kwa kuwaletea mradi mkubwa wa shule ya Sekondari ambapo hawakuwa nayo awali
Awali wakazi hao wa Bunda mjini waliiambia Mazingira FM kuwa walitamani sana kuwa na shule lakini changamoto ilikuwa ni kutokuwepo na eneo la kujenga shule hiyo.