Mabotto kuwasomesha wanafunzi watakaofaulu kwa daraja la kwanza
19 October 2023, 9:17 pm
Mbunge Robert Maboto ameahidi kuwafadhili vifaa vya shule wakati wa kujiunga na kidato cha Tano wanafunzi wote shule ya Sekondari Wariku na Dr. Nchimbi watakaopata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani wa taifa unaotarajiwa kifanyika mwezi November mwaka huu.
Na Adelinus Banenwa Na Edward Lucas
Mbunge Robert Maboto ameahidi kuwafadhili vifaa vya shule wakati wa kujiunga na kidato cha Tano wanafunzi wote shule ya Sekondari Wariku na Dr. Nchimbi watakaopata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani wa taifa unaotarajiwa kifanyika mwezi November mwaka huu.
Ahadi hiyo imetolewa na Emmanuel Kija katibua wa mbunge katika mahafali ya 16 kidato cha nne shule ya sekondari Wariku iliyopo kata ya Wariku wilayani Bunda ambapo alifika kumuwakilisha mgeni rasmi Mhe Mabotto.
Aidha katika hatua nyingine kiasi cha shilingi milioni moja na elfu kumi zimetolewa na mbunge huyo katika ukamilishaji wa ujenzi wa choo shule ya sekondari Wariku iliyopo halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara
Fedha hizo zimetolewa na katibu wa mbunge wa jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija katika mahafali hiyo ya kidato cha nne ya shule hiyo ambapo amesema Mhe mbunge kipaumbele chake katika jimbo ni suala la elimu ndo maana kupitia fedha za mfuko wa jimbo na hata fedha zake binafsi kwa kiasi kikubwa anazielekeza kwenye sekta ya elimu.
Bwire Mashauri mkuu wa shule ya sekondari wariku amesema shule hiyo imepata mafanikio mengi hasa ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuhitimu hivi karibuni ikiwemo mwanafunzi mmoja kupata daraja la kwanza ya alama nane katika mtihani wa halmashauri ya mji wa bunda
Aidha amesema pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto mbalimbali zinazokabili shule hiyo ikiwemo ushirikiano duni kutoka kwa wazazi, wazazi kutofuatilia maendeleo ya watoto wao utoro wa wanafunzi unaosababishwa na wazazi miongoni mwa changamoto zingine.
Awali wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wanafunzi wahitimu wamesema walianza kidato cha kwanza wakiwa jumla ya wanafunzi 140 lakini kutokanana na changamoto mbalimbali wanahitimu wanafunzi 87 wavulana 43 na wasichana 44.
Aidha wamesema kuna baadhi ya chanagamoto za ukosefu wa maji safi na salama shuleni hapo, upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi upungufu wa matundu ya vyoo miongoni mwa changamoto zingine.