Uchechemuaji katika masuala ya kilimo ni muhimu
22 September 2023, 2:26 pm
Kupitia mradi wa ASILI-B unaofadhiliwa na Vi Agroforestry, CSP kwa kushirikiana na BUFADESO wamewakutanisha wadau wa kilimo wilaya ya Bunda na kuunda jukwaa la kilimo.
Na Thomas Masalu
Kupitia mradi wa ASILI-B unaofadhiliwa na Vi Agroforestry, CSP kwa kushirikiana na BUFADESO wamewakutanisha wadau wa kilimo wilaya ya Bunda na kuunda jukwaa la kilimo la wilaya ambalo litatekeleza kazi mbalimbali ikiwa pamoja kupandisha utashi wa kisiasa kwenye sekta ya kilimo, kutathmini na kufuatilia bajeti za kilimo katika halmashauri, kuwajasirisha wakulima kuwafanya watendaji wawajibike.
Jukwaa hilo litafanya kazi zake kupitia Uchechemuzi wa masuala ya Kilimo ili kuwa na sera zenye kukidhi mahitaji ya sekta ya kilimo.
Akizungumza na radio Mazingira mkurugenzi mtendaji wa shirika la CSP Ndugu Nemence Iriya amesema lengo kuu la programu ya ASILI-B ni kuboresha usalama wa chakula na lishe kwa wakulima wadogo, maisha endelevu, usawa wa kijinsia, na ustahimilivu.
Aidha Iriya amesema kupitia mradi huo pia wataimarisha uhifadhi wa bayoanuai na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.