Wananchi wa Tamau wapata kivuko kipya kilichogharimu 420000/Tsh
19 October 2021, 5:26 pm
Uongozi wa serikali ya mtaa wa Tamau kata ya Nyatwali Halmashauri ya mji wa Bunda leo umekabidhi kivuko kipya kwa wananchi wa eneo la Tamau ujaluoni ili kurahisisha shughuli za uvukaji katika eneo hilo.
Akikabidhi mtumbwi huo uliogharimu kiasi cha shilingi 420,000 Afisa mtendaji mtaa wa Tamau, Kihiri Mirumbe amesema pesa hiyo imepatikana baada ya serikali ya mtaa kutoa shilingi 320,000 na Mbunge wa Jimbo la Bunda mjini Robert Maboto kuchangia shilingi laki moja.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Tamau, Asafu Ernest Owiti amesema mtumbwi huo utasaidia kupunguza adha ya uvukaji katika eneo hilo kwani kwani kivuko kilichokuwepo kilikuwa kimechakaa jambo lililokuwa linahatarisha usalama wa wananchi hao.
Aidha amewata wananchi wananchi kukitumia vizuri kivuko hicho ili kiweze kudumu na kuwasaidia katika changamoto ya uvukaji huku akiahidi kukifanyia marekebisho kivuko cha zamani na mpango wa mbunge kuwatafutia kivuko kingine.
by Edward Lucas