Nassar:-Ruwasa simamieni suala bili za Maji ili mpanue mtandao wa maji
8 October 2021, 3:59 pm
Jumuiya za watumiaji maji wilaya ya Bunda Mkoani Mara wametakiwa kusimamia ipasavyo miradi ya maji iliyo katika maeneo yao kwa kuhakikisha wanatumia vizuri pesa wanazo kusanya katika miradi hiyo.
Agizo hilo limetolewa leo Oct.7. 2021 na mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Bunda Mh. Joshua Nassari wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya maji wilaya ya Bunda uliosimamiwa na wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini RUWASA ikiwa na lengo la kujadili namna ya kuhakikisha huduma ya maji vijijini inapatika kwa uhakika.
Mh. Nassari amesema fedha zote zinazokuswanya na jumuiya ya maji kutokana na bili ya maji zinatakiwa zibaki ili kutanua mtandao wa maji ndani yao
Aidaha amezitaka jumuiya hizo kuhakikisha wanahimiza wananchi kufunga maji kwenye miji yao ili kuendana na sera ya Serikali ya kuhakikisha kila mtu anapata maji safi na salama
Akitoa salamu kwa wadau wa sekta ya maji kwenye mkutano huo muwakilishi wa meneja wa RUWASA mkoa wa Mara afisa utumishi Stanley Sing’ira amebainisha kuwa lengo la RUWSA ni kuhakikisha mamlaka hiyo inatoa huduma ya maji kwa wananchi huku akiendelea kusisitiza jumuiya za maji.
By Thedy Thomas