Siku ya Mwalimu Duniani: walimu waaswa kuendelea kusimamia nidhamu na elimu
5 October 2021, 4:50 pm
Wito umetolewa kwa walimu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara kuendelea kusimamia nidhamu, elimu kwa wanafunzi na kuelimisha jamii inayo wazunguka hasa katika masuala ya ujenzi wa Taifa.
Wito huo umetolewa leo na katibu msaidizi wa Tume ya utumishi wa walimu wilaya ya Bunda mwl. Magesa Protas kwenye kipindi cha Duru za habari kupitia redio Mazingira fm kuelekea siku ya Mwalimu Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 5 Oct kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Mwalimu ni kiini cha kuhuisha elimu”
“Wito wangu kwa walimu tuendelee kusimamia nidhamu,tuendelee kusimamia elimu kwa wanafunzi na tuendelee kuelimisha jamii inayotuzunguka kwa sababu sisi walimu tunazo kazi nyingi na si kufundisha pekeyake, tunapokuwa kwenye jamii tunafundisha watoto na kuelimisha jamii inayo tuzunguka” alisema mwl. Magesa Protas katibu msaidizi wa Tume ya utumishi wa Walimu wilaya ya Bunda.
Katika hatua nyingine Mwl. Magesa amesema wamekua wakishirikiana na serikali kuhakikisha Sera mbalimbali za Serikali zinakwenda na kuhakikisha mipango ya Serikali haikwami.
By Therezia Thomas