Dampo lawa kero kwa wakazi wa Migungani kata ya Bunda stoo
6 July 2021, 6:35 pm
By Adelinus Banenwa
Wananchi wa mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda wameiomba serikali kuhamisha dampo la Migungani kutokana na kero kubwa wanazozipata
Hayo wameyasema leo july 5, katika eneo la dampo la maji taka wakati wakizungumza na Redio Mazingira FM wananchi hao wamesema dampo hilo lipo katikati ya makazi ya watu pia shimo la maji taka limejaa
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bunda stoo Mh Flavian Chacha amesema atawasiliana na serikali pamoja na wataalam wa afya pia kupeleka hoja kwenye baraza la madiwani ili dampo hilo liweze kuhamishwa kwenye makazi ya watu na kutafutiwa sehemu nyingine
Naye afisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Amani Jumbula amesema uwepo wa dampo hilo ni hatari kwa afya za wananchi hivyo amemuagiza afisa afya wa mtaa kuandika tathimini ya afya ya dampo hilo kama mapenekezo kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi hao