Diwani wa bunda stoo atoa mifuko 5 ya saruji ujenzi wa choo shule ya miembeni
7 June 2021, 5:53 pm
Diwani wa kata ya Bunda Stoo Flavian Chacha ametoa mifuko mitano ya saruji katika kuunga juhudi za wananchi za ujenzi wa choo cha shule ya msingi miembeni
Katika ujumbe wake diwani huyo amesema ameona ni vyema kushiriki juhudi za wananchi kwenye ujenzi huo wa choo kwa kuwa hapendi kuona shule inafungwa kwa kukosa choo hivyo anawaomba wadau wengine kuendelea kujitolea kuisaidia serikali na wananchi ili kulenta maendeleo kwa jamii
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni A David Magesa amesema shule ya miembeni yenye A na B kuna jumla ya wanafunzi 2500 hivyo uhitaji wa vyoo kwa shule zote mbili A na B ni zaidi ya matundu 100 hivyo amemshukuru diwani kwa kujitolea kuchangia maendeleo ndani ya kata yake
Naye mwenyekiti wa ujenzi wa choo hiyo ndugu Emmanuel Nyamonge amesema ujenzi huo ulianza mwezi wa tisa mwaka jana na juhudi za wananchi zinatumika ambapo kila kicha cha mtoto huchangia kiasi cha shilingi 5500 na ujenzi huo umepagwa kugharimu shilingi milioni 12 ambapo mpaka sasa imepatikana shilingi million 4 tu