Wananchi wa kata ya Hunyari Bunda kulipwa kifutajasho
18 May 2021, 5:42 pm
Serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii imetenga zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kulipa kifuta jasho kwa wananchi waliofanyiwa uharibifu wa wanyamapori katika mashamba na makazi wanayoishi katika vijiji vitatu Mariwanda,Hunyari na Kihumbu vilivyopo Bunda Mkoani Mara
Hayo yamesemwa na waziri wa Maliasili na utalii Dk.Damas Ndumbaro wakati alipofanya ziara yake ndani ya wilaya ya Bunda na kuzungumza na wananchi wa kata ya Hunyari ambayo ina vijiji vitatu nakuahidi kulipwa kifuta machozi kwa wale wote waliofanyiwa uharibifu na wanyamapori
Majibu hayo yalikuja muda mfupi baada ya wananchi kulalamikia swala la kifuta jacho huku taarifa ya wilaya iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Bunda mwl.Lydia Bupilipili ikieleza changamoto zinazowakabili wananchi wake mojawapo likiwemo swala la uharibifu unaosababishwa na wanyamapori
Mara baada ya maagizo ya waziri wa maliasili na utalii kutajwa kuwepo kwa pesa hiyo ya kifuta jasho, bila kupepesa macho amesema pesa hiyo itakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ndani ya wiki mbili zijazo na mchakato wa kuanza kuzigawa utaanza hivyo aliomba majina ya wanaohitaji kulipwa fidia kufikisha majina yao mapema ili walipwe kwa kufuata utaratibu maalum