Milion 7 kujenga choo genge la jioni Bunda
16 April 2021, 6:54 pm
Mwenyekiti wa wajasiliamali mkoa wa mara Charles Waitara amewashukuru Mbunge wa Bunda Mjini Robert chacha maboto, Diwani wa Bunda Mjini pamoja na Mkurungenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kuadhimia kujenga choo eneo la genge la jioni
Waitara ameyasema hayo leo April 16 .2021 kwenye kikao cha hadhara na wajasiliamali wadogo kilichofanyika maeneo ya genge la jioni Mjini Bunda na kuainisha kuwa genge la jioni lina maitaji mengi lakini suala la choo ilikuwa ni changamoto kubwa sana
Naye Diwani wa kata ya Bunda Mjini Mzamil Ibrahim amesema zimetengwa million saba kwa ajili ya ujenzi wa choo katika genge hilo na mchakato umeanzahivyo yeye kwa kushirikiana na Mbunge wataakikisha wanaleta maendeleo kwa watu bila ubaguzi
Aidha wananchi wamebainisha uhitaji uliokuwepo wa choo katika genge hilo na wanaupokeaje ujenzi wa choo hiyo katika maeneo yao ya biashara zao