

2 April 2021, 5:27 pm
Taarifa ya kupokea pesa hizo imetolewa katika kikao cha baraza la madiwani kwenye kikao cha robo ya pili ya Mwaka na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Staffa Nashon
Hata hivyo Nashon amewaomba waheshimiwa madiwani kuacha malumbano ya wapi halmashauri hiyo ijengwe na badala yake wajielekeze kwenye ujenzi ili waweze kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Halmashauri ya wilaya ya Bunda ilipokea Barua kutoka ofisi ya katibu mkuu TAMISEMI ikielekeza kujengwa makao makuu ya halmashauri hiyo eneo la Kibara stoo kata ya Kibara Tarafa ya Nansimo.