Bunda; ahukumiwa kifungo cha maisha jela na fidia ya shilingi milioni moja kwa kosa la kubaka
29 November 2022, 12:37 pm
Mahakama ya wilaya ya Bunda imemuhukumu kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja Steven Mwita 52 mkazi wa mtaa wa Kinyabwiga kata ya Guta halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara kwa kosa la kubaka.
Hukumu hiyo imetolewa leo 29 NOV 2022 katika mahakama ya Bunda.
Mwendesha mashtaka Tryphone Makosa Jacob mkaguzi msaidizi wa polisi amesema mnamo tarehe 18 mwezi wa 10 mwaka 2022 majira ya saa saa kumi na mbili za jioni katika eneo la Kunanga mtaa wa Kinyambwiga kata ya guta wilayani Bunda mtuhumiwa Steven Mwita (52) mkulima alimbaka mtoto wa miaka 9 jina limehifadhiwa mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kunanga.
Tryphone amesema mtuhumiwa alikutana na mtoto huyo njiani na kumwamnbia waongozane ili akamuagize sehemu ila walipofika mbele kidogo alimvuta kwenye mahame ( nyumba zilizotelekezwa) kisha kumvua nguo na kumbaka huku akiwa amemziba mdomo asipige kelele na baada ya kufanya kitendo hicho alikimbia.
Tryphone ameongeza kuwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo angali akijua ni kinyume cha sheria 130 (1) na (2) (e) na 131 (3) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 toleo la mwaka 2022. Na kuomba mahakama itoe adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hizo.
Mtuhumiwa alikiri makosa yote baada ya kuulizwa huku akiiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ni mara yake ya kwanza kutenda kosa hilo.
Hakimu mkazia mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda Mulokozi Paschal Kamuntu amesema baada ya kusikiliza pande zote amejilidhisha pasipo na shaka na kwa kuwa mtuhumiwa amekiri makosa na kwa kuwa kosa alilolifanya mtuhumiwa kumbaka mtoto chini ya miaka kumi adhabu yake ni moja tu ya kifungo cha maisha jela.
Hivyo amemuhukumu kifungo cha maisha jela na kumlipa fidia ya shilingi million moja.
BY Adelinus Banenwa