Mazingira FM

Baraza la Madiwani Bunda; Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Magafu Manumbu ameagiza ujenzi wa madarasa ya Sekondari uende haraka

11 November 2022, 1:48 pm

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Magafu Manumbu ameagiza utekelezaji wa ujenzi wa madarasa ya Sekondari uende haraka na kama Kuna changamoto zozoto waseme haraka ili ndani ya mwezi December ujenzi uweze kukamilika.


Manumbu ameyasema hayo katika Kikao Cha kawaida cha robo ya kwanza Cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mwaka 2022/2023

Manumbu ameongeza kuwa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Bunda unasuasua ambapo amesema pamoja na matatizo mengine maji yalikuwa tatizo

 

kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bunda Ndugu. Mayaya Abraham Magesse amesema anaipongeza Tarura kwa Kazi nzuri wanayoifanya kwa kuchonga barabarani za mitaan

 

Pia amesema mambo yanayosemwa kuhusu Halmashauri ya wilaya ya Bunda hayana Afya kwa kuwa kila Mahali kuna taarifa za miradi mingi yenye ukakasi hivyo kila mtu anatakiwa kutimiza wajibu

Amesema kwa sasa dunia ipo kiganjani hivyo kila mtu anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa kuwa taarifa anazipata kupitia vyombo vya habari na kupitia bungeni kwa maana miradi inayoletwa na serikali wananchi wanaitazama kwa karibu.