Mazingira FM

DC Nassar awaita ofisini kwake viongozi wa kata kueleza kwa nini hawajaanza ujenzi wa madarasa wakati fedha zipo kwenye akaunti zaidi ya mwezi mzima

2 November 2022, 7:42 pm

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Joshua Nassar ameagiza uongozi wa kata ya Nyamang’uta kufika ofisini kwake ili kutoa maelezo kwa nini hadi sasa hawajaanza ujenzi wa darasa hata Moja Kati ya Madarasa Saba yanayotakiwa kujengwa kutokana na fedha zilizotolewa na serikali.

Mhe Nassar ametoa maagizo hayo katika ziara yake Wilayani Bunda katika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Madarasa ya shule za Sekondari kwa ajili ya wanafunzi wa kidato Cha kwanza 2023

“Tangu mpate fedha hizo hakuna kiashilia chochote ambacho kimeletwa hapa wakati wenzenu huko tayari wameanza kupandisha Kuta za Madarasa Halmashauri ile ile fedha zilitolewa kwa pamoja, Wilaya ile ile, Mkurugenzi yule yule, afisa elimu yule yule. Ninyi shule ya nyamang’uta mnatatizo Gani? Maelekezo yangu nataka kesho tarehe 3 Nov sambili Asubuhi uongozi wa Shule na kata kufika ofisini kwa DC kuniambia kwa nn mnazolota kwenye utekelezaji wa miradi hii”.

Kwa upande wake mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari nyamang’uta amesema tatizo kubwa ni Baadhi ya viongozi wa kata kuingilia ujenzi wengine wakitaka zabuni za kuleta viashilia

Shule hiyo ya Nyamang’uta imepata fedha za ujenzi wa madarasa saba ambapo kwa mujibu wa afisa elimu sekondari halmashauri ya wilaya ya Bunda fedha hizo ziliingia kwenye akaunti za shule tangu 31 sep 2022 lakini hadi ziara ya mkuu wa wilaya  shule hiyo ilikuwa haijui wapi ijenge madarasa hayo.