Halmashauri ya Mji wa Bunda yapokea tani 30 za mahindi ya bei nafuu
13 September 2022, 7:49 am
Halmashauri ya Mji wa Bunda imepokea tani 30 za mahindi ya bei nafuu kutoka kwa wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa NFRA
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Katibu tawala Wilaya ya Bunda Salum halfani Mterela amesema mahindi yaliyoletwa ni kwa ajili ya wananchi wa kawaida kwa ajili ya chakula
Mterela ametoa ufafanuzi kuwa kilo Moja ya mahindi itauzwa kwa shilingi 920 huku akisisitiza kuwa mwananchi anayetaka kununua kuanzia gunia Moja yaaani kilo 100 anatakiwa awe na uthibitisho wa barua ya afisa mtendaji
Aidha ametoa onyo Kali kwa wafanyabiashara kutojiingiza kwenye ununuzi wa mahindi hayo kwa namna yoyote kwa kuwa mbinu zote wanazozitumia wameishazibaini hivyo wazingatie kwamba mahindi haya ni kwa ajili ya chakula kwa wananchi
Ametoa Rai kwa wananchi kutokubali kutumiwa na wafanyabiashara ili lengo la serikali liweze kufikiwa
Mterela amesema mahindi hayo yanapatika katika stoo ya Bunda mjini iliyopo karibu na shule ya msingi Miembeni