Bunda: wananchi waonywa uhujumu wa miondombinu ya maji
24 August 2022, 8:40 pm
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji Bunda eng maisha amewataka wakazi wa Mji wa Bunda kuacha kuhujumu miundombinu ya maji ili kuebusha hasara kwa mamlaka na serikali
Akizungumza na redio Mazingira Fm ofisini kwake eng maisha amesema matukio ya watu kukata mabomba ya maji yanashamili sana hasa kipindi Cha kiangazi na wahusika wengi ni wale wanaofyatua tofali na kunywesha mifugo hivyo kusababisha hasara kwa mamlaka hiyo
Amesema hadi hivi sasa mamlaka ya maji Bunda inawahudumia watumia maji 6500 ndani ya Mji wa Bunda huku akiwataka wananchi kutoa taarifa za uhujumu wa miundombinu hiyo kama vile tutobolewa kwa Bomba miongoni mwa matukio mengine
Aidha amewataka wananchi wanaotaka kuunganisha maji kwenye majumba Yao kufika ofisi za mamlaka ya maji kufuata utaratibu unaelekezwa na kuepukana na vishoka wa mtaani