

7 April 2025, 8:50 pm
Mwananchi kushawishi mgombea au mtia nia kumpatia chochote ni kinyume na sheria ya takukuru sura ya 329 kifungu cha 15 (8)
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa hasa kwa kuwashawishi viongozi na watia nia kuwapatia vitu kwa lengo la kuwakubali
Wito huo umetolewa na maafisa wa TAKUKURU kutoka mkoa wa mara walipozungumza kwenye kipindi cha ufahamu wa sheria kinachorushwa hapa radio Mazingira Fm
Zena Kisesa mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoa wa Mara amesema kwa namna yoyote ile mwananchi kushawishi mgombea au mtia nia kumpatia chochote ni kinyume na sheria ya TAKUKURU sura ya 329 kifungu cha 15 (8) na adhabu yake ni sawa na yule aliyetoa ama kupokea rushwa.
Naye Winfrida Kanyika afisa TAKUKURU mkoa wa Mara amesema kitendo cha wananchi kuomba au kushawishi kupewa rushwa kinamnyima mwananchi uhuru wa kumchagua kiongozi bora hivyo wagombea wanadi sera zao na wananchi wasiwe chanzo cha kuomba rushwa,