Mazingira FM

Zahanati ya Mcharo yafungwa miezi miwili kwa kukosa Choo

25 April 2022, 9:07 am

Choo cha Mcharo iliyosababisha Zahanati kufugwa

Ni miezi miwili tangu kufugwa kwa zahanati ya mcharo iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Wakizungumza na redio Mazingira Fm Baadhi ya wakazi wa Mcharo wamesema tangu kufugwa kwa choo hiyo wanateseka sana hasa huduma za mama na mtoto

“Ni miezi miwili sasa tangu zahanati hii ifungwe tunateseka sana huduma tunazipata Bunda Mjini au Sazira nauli zimepanda kwenda na kurudi  Sazira  shilingi 6000 na kwenda na kurudi Bunda Mjini shilingi 8000 nani anaweza ghalama hizi?” Amesema Loveness Nzagi

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mcharo Charles Bupumula amesema wananchi wa Mcharo walianza kuchangia katika ujenzi wa choo nyingine lakini Nguvu zao hazikutosheleza mahitaji ambapo tathmini  ya ujenzi ilikuwa shilingi milion mbili na laki Tano sh. 2,500,000/=

Bupumula ameongeza kuwa Mh Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Robert Chacha Maboto amewaunga mkono wananchi wa Mcharo kwa kuchangia fedha za ujenzi wa choo

Kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Robert Chacha Mabotto, Katibu wa Mbunge Peluth Mwita amesema baada ya ofisi ya Mbunge kupokea ombi la kuchangia ujenzi wa choo ya Mcharo Mh Mbunge ametoa shilingi “Milion Moja laki Tano na elfu tisa”  Sh. 1,509,000/= .

Choo mpya inayojengwa katika Zahanati ya Mcharo baada ya choo ya awali kutokidhi sifa na kusababisha Zahanati kufugwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mh Emmanuel Mkongo amesema baada ya kupata taarifa za kufugwa kwà zahanati ya Kata ya Mcharo kwà sababu za choo kutokukidhi, alielekeza zahanati hiyo ifunguliwe wakati mambo mengine yanafanyiwa kazi.

By Adelinus Banenwa