Vitambulisho elfu 12 vyakwama ofisi za NIDA Bunda
22 January 2025, 1:05 pm
Vitambulisho elfu 12 ni kati ya vitambulisho 62,370 vilivyoletwa Bunda.
Na Adelinus Banenwa
Afisa usajili mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA wilaya Bunda Fredson John Samwel amesema zaidi ya vitambulisho elfu 12, vimerejeshwa ofisi za NIDA wilaya kutoka kwenye ofisi za vijiji na mitaa kutokana na kukaa muda mrefu kweye ofisi hizo bila kuchukuliwa na wahusika.
Ndugu Fredson amesema hayo kwenye kipindi cha Asubuhi kupitia Radio Mazingira fm ambapo amesema jumla ya vitambulisho 62,370 vililetwa Bunda na kati ya hivyo vitambulisho 53,850 vimechukuliwa ambapo NIDA pia iliongeza vitambulisho 6,779 hivyo vitambulisho vilivyokuwa vimesalia ni zaidi ya vitambulisho 12,000
Katika hatua nyingine Fredson amesema kila mwenye kitambulisho chake wilayani anatumiwa ujumbe mfupi wa sms kwa namba yake mpya hata kama namba uliyoweka namba tofauti
Aidha ameongeza kuwa mtu yeyote asiende kwa ofisi za NIDA kufuata kitambulisho ikiwa hajapata ujumbe kwenye simu yake wa kumtaka kwenda.
Pia Fedson amesema inaruhusiwa mtu kumuagiza ndugu yake kumchukulia kitambulisho kwa kumtumia ujumbe aliyotumiwa na NIDA ambao ujumbe huo unathibitishwa na maafisa wa NIDA kabla ya kumpatia kitambulisho hicho.