Wanasheria wa Rais Samia watua Bunda
13 December 2024, 7:08 am
Changamoto za kisheria zilizopo wilayani Bunda ni tatizo la migogoro ya ardhi, mirathi n.k.
Na Adelinus Banenwa
Wananchi wilayani Bunda wametakiwa kujitokeza na kutumia fursa ya timu ya wataalamu wa sheria kutoka kwa Rais Samia inayozunguka kusikiliza kero, ili kutatua changamoto zao za kisheria.
Hayo yamesemwa na katibu tawala wilaya ya Bunda ndugu Salumu Mtelela kwa niaba ya Mhe mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano ambapo amesema timu hiyo tayari imeshawasili Bunda na kuanza kazi katika maeneo mbalimbali hivyo wananchi wasisite kupeleka kero zao za kisheria.
Mtelela ameongeza kuwa miongoni mwa changamoto za kisheria zilizopo wilayani Bunda ni tatizo la migogoro ya ardhi, mirathi miongoni mwa changamoto zingine ambapo rai yake ni wananchi wote wenye kero za aina hiyo kukutana na timu hiyo ili waweze kupata msaada.