Mazingira FM

TANAPA Kanda ya Magharibi yatoa vifaa kwa bodaboda Bunda

3 October 2024, 7:38 pm

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akipokea refractor kutoka kwa Albert Mziray  ambaye ni  msimamizi wa  kitengo cha uhifadhi na maendeleo ya biashara TANAPA kanda ya magharibi

TANAPA wamesaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli za maendeleo katika jamii ikiwemo utengenezaji madawati, ujenzi wa zahanati, madarasa miongoni mwa  kazi zingine.

Na Adelinus Banenwa

TANAPA Kanda ya Magharibi itoa refractor  1000 kwa waendesaha pikipiki maarufu bodaboda wilayani Bunda.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano leo Oct 3, 2024 ofisini kwakwe, Albert Mziray  ambaye ni  msimamizi wa  kitengo cha uhifadhi na maendeleo ya biashara TANAPA kanda ya Magharibi kwa niaba ya kamishna wa TANAPA kanda hiyo mziray amesema wameamua kufanya hivyo ili kusaidia vijana kuepukana na ajari.

Mziray ameongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya ujirani mwema ambapo TANAPA wamekuwa wakitoa kwa jamii inayozunguka hifadhi na misaada hiyo ni muendelezo.

Sauti ya Albert Mziray  ambaye ni  msimamizi wa  kitengo cha uhifadhi na maendeleo ya biashara TANAPA kanda ya Magharibi

Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Bunda DKT Vicent Naano amewashukuru TANAPA  kwa kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia jamii huku akibainisha kuwa huo ndiyo umuhimu wa kuwa na wanyamapori na hifadhi karibu.

Dc Naano amesema TANAPA wamesaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli za maendeleo katika jamii ikiwemo utengenezaji madawati, ujenzi wa zahanati, madarasa miongoni mwa  kazi zingine.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bunda DKT Vicent Naano