Vijiji 389 Bunda DC kushiriki uchaguzi serikali za mitaa
27 September 2024, 1:20 pm
Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Bunda George Stanley Mbilinyi, Picha na Adelinus Banenwa
Kwa mujibu wa kifungu cha 57 cha sheria ya serikali za mitaa sura ya 287 na kifungu cha 16 cha serikali za mitaa sura 288 uchaguzi kufanyika kila baada ya miaka 5.
Na Adelinus Banenwa
JUMLA ya vitongoji 389 ,vijiji 78 na kata 19 za halmashauri ya wilaya ya Bunda zinatarajia kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika , November 27 2024.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya BUNDA ,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Bunda George Stanley Mbilinyi amesema kwa mujibu wa kifungu cha 57 cha sheria ya serikali za mitaa sura ya 287 na kifungu cha 16 cha serikali za mitaa sura 288 uchaguzi kufanyika kila baada ya miaka 5.
Aidha Mbilinyi ametaja viongozi wenye sifa za kushiriki katika uchaguzi pamoja na nafasi za uongozi zinazogombewa kuwa ni pamoja na wenyeviti serikali za Vijiji, Vitongoji na wajumbe wa maeneo hayo.
Mbilinyi amesema zoezi la uandikisha daftari la makazi litafanyika kati ya tarehe 11 October hadi 20 October 2024, pia zoezi la uchukuaji wa fomu kwa wagombea litakuwa kati ya tarehe 1- 7 November 2024 na pia na muda wa kampeini ni siku saba ambazo ni kati ya tarehe 20 hadi 26 November 2024.
Sambamba na hayo pia Mbilinyi amewataka viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wazee maarufu pamoja na wadau wengine wote kushirikiana kutoa elimu kwa wananchi kujitokeza katika kujiandikisha.
Mkutano huo umehudhuriwa na watendaji wa kata ,watendaji wa vijiiji,viongozi wa siasa ,viongozi wa dini, pamoja na wakuu wa idara wote kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda.