Mazingira FM

Kampuni ya ukopeshaji Bunda yakamatwa na kadi za benki zaidi ya 50

18 September 2024, 7:04 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akizungumza na wakazi wa Nyatwali baada ya kukamata kampuni ya ukopeshaji iliyokuwa inataka kuwadhurumu wakazi wa Nyatwali baada ya kulipwa fidia

“Mimi kama mkuu wa wilaya ya Bunda siwezi kukubali ujambazi kama huu wa kuwadhurumu wananchi haiwezekanai mtu akope milioni moja alafu alipe milioni kumi huu ni ujambazi” DC Vicent Naano.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano amekamata vijana wa kampuni iliyokuwa imewakopesha fedha wakazi wa nyatwali na kuwawekea riba kubwa kinyume na sheria za mikopo.

Dc Naano ameselielekeza jeshi la polisi kushirikiana na TAKUKURU kuwahoji watuhumiwa waliokutwa na nyaraka za wakazi wa nyatwali ikiwemo kadi za benk zaidi ya 50 na fomu namba tatu zinazotumika kuchukulia hundi zaidi ya 60.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akizungumza na wakazi wa Nyatwali baada ya kukamata kampuni ya ukopeshaji iliyokuwa inataka kuwadhurumu wakazi wa Nyatwali baada ya kulipwa fidia

Mkuu wa wilaya amesema akiwa katika nafasi yake hawezi kukubali ujambazi wa namna hiyo ambapo ameeleza kusikitishwa na jambo hilo ambapo miongoni mwa fomu zilizokamatwa ni fomu ya bibi kizee ambaye fidia yake ni milioni 7 na alikopa shilingi milioni 1 lakini kampuni hiyo ya ukopeshaji inataja kumdai bibi huyo kiasi cha shilingi milioni 10.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akizungumza na wakazi wa Nyatwali baada ya kukamata kampuni ya ukopeshaji iliyokuwa inataka kuwadhurumu wakazi wa Nyatwali baada ya kulipwa fidia
Sauti ya DC Naano

Dc Anney ameongeza kuwa kwenye ukopeshaji wake kampuni hiyo ambayo hakuitaja jina ilikuwa inawakopesha wakazi wa nyatwali bila kuwaambia kiasi cha riba pia inatatwa kugushi muhuri wa wakili uliotumika kwenye fomu za mikopo

Sauti ya DC Naano