Zaidi ya miche ya miti milioni moja imepandwa Bunda DC
9 September 2024, 4:21 pm
Takribani miche ya miti million moja na elfu ishiri tayari imepandwa katika maeneo mbalimbali ya halimashauri ya wilaya ya Bunda
Na Catherine Msafiri
Takribani miche ya miti million moja na elfu ishiri tayari imepandwa katika maeneo mbalimbali ya halimashauri ya wilaya ya Bunda ili kuhakikisha wanatunza mazingira na kuhifadhi mistu.
Hayo yamebainishwa na afisa maliasili na usimamizi wa mazingira kutoka halmashauri ya wilaya ya Bunda ndugu. Marwa Paul Kitende wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha uhifadhi na utalii cha radio Mazingira FM kuhusu umuhimu wa misitu kwa jamii na mazingira
Aidha amebainisha kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuhifadhi mistu kwani husaidia katika mambo mbalimbali hasa suala la mabadiliko ya tabianchi,kuongeza mazalia ya samaki,kuna miti ya dawa ,chakula nakadhalika
Ndugu.kitende ameongeza kuwa wao kama ofisi ya maliasili na usimamizi wa mazingira wanatoa ushauri juu ya miti gani sahihi ya kupanda kwa kuzingatia mahitaji lakini pia wanashauri matumizi ya majiko banifu ili kupunguza mahitaji makubwa ya ukataji miti
Kwa upande wake katibu wa shirika la COSUDE Ndugu, Flavian Ernest Nyanza ameeleza mikakati walionayo wao kama shirika katika kuhakikisha wanasaidia suala la uhifadhi wa misitu na mazingira kwa ujumla
Huku akiiomba serikali kuhakikisha wanasaidia kuwawezesha wanavikundi wanaofika kupata mikopo wasipewe pesa badala yake wapewe mashine za kuzalisha nishati ya kupikia ili kuepuka ukataji wa miti kwaajili ya kuni na mkaa.