DC Bunda; “Muacheni mkaguzi wa ndani afanye kazi yake”
9 September 2024, 4:10 pm
Mkuu wa wilaya ya Bunda ameelekeza halmashauri ya wilaya ya Bunda kumuacha mkaguzi wa ndani kufanya kazi yake.
Na Adelinus Banenwa
Mkuu wa wilaya ya Bunda ameelekeza halmashauri ya wilaya ya Bunda kumuacha mkaguzi wa ndani kufanya kazi yake.
Huku akimtaka mkaguzi wa ndani kuhakikisha kila mwezi anapeleka taarifa ya hoja alizozibaini na kuhakikisha hoja hizo zinapatiwa majibu.
Amesema awamu hii haitakiwi kukutana na hoja za CAG sabini na kuendelea badala yake wakutane na hoja za kisera ambazo haziihusu halmashauri na hili litafanikiwa endapo mkaguzi wa ndani atafanya kazi yake na kazi yake kufanyiwa kazi na halmashauri likiwemo baraza la madiwani.
Ameongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Bunda ni miongoni mwa halmashauri nchini zenye hoja nyingi za ukaguzi.