Diwani Keremba achaguliwa tena makamu mwenyekiti Bunda DC
9 September 2024, 4:00 pm
Baraza la madiwani Bunda DC lamchagua tena Keremba Irobi diwani kuwa mwenyekiti wa halmashauri kwa mara ya nne mfururizo.
Na Adelinus Banenwa
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda limemchagua diwani wa kata ya Nyamang’uta Mhe Kilemba Irobi Kilemba kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Uchaguzi huo wa makamu mwenyekiti umefanyika leo tarehe 6 Sept 2024 kwenye kikao cha mwaka cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Mhe Kiremba amechaguliwa kwa mara ya nne mfururizo ambapo leo amepata kura 21 kati ya kura 23 zilizopigwa na kura mbili zikiwa za hapana.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo yaliyokuwa na matokeo ya hapana au ndiyo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Magafu Manumbu amesema: