Mazingira FM

DC Naano, aipongeza halimashauri ya Bunda DC ukamilishaji wa miradi tofauti na zamani

9 September 2024, 12:38 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano, Picha na Adelinus Banenwa

“Mwenyekiti nawapongeza mmejitahidi ukusanyaji wa mapato mwaka wa fedha 2023 na 2034 endeleeni kushirikiana”

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano Ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Bunda kwa ukusanyaji wa mapato na ukamilishaji wa miradi kwa wakati  tofauti na awali.

Akizungumza katika kikao cha mwaka cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano amesema ni jambo la kupongeza kuona hilo limefanikiwa.

sauti ya DC Naano

Amewataka halmashauri ya kusimamia mifumo ya manunuzi hasa mfumo wa sasa wa manunuzi na tenda NEST kusimamia suala la bei elekezi na upatikanaji wa wazabuni na mafundi .

Baadhi ya madiwani kwenye baraza la robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023 na 2024 halamshauri ya wilaya ya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Aidha ameielekeza halmashauri ununuzi wa vifaa kwa kuzingatia hatua za ujenzi ambapo amepainisha katika baadhi ya maeneo kununuliwa kwa vifaa vya umeme angali huduma na mfumo wa umeme kabla haujafungwa katika mradi huo.

sauti ya DC Naano

Sambamba na hayo pia Mhe Anney ameitaka halmashauri ya wilaya ya Bunda kununua vifaa kulingana na mahitaji ya jengo au mradi husika huku akisisitiza thamani ya fedha kulingana na mradi husika