Maboto kutoa bima za afya kwa wazee 198 Bunda
15 June 2024, 9:26 pm
Wazee 198 Bunda mjini kunufaika na bima ya afya kutoka kwenye mshahara wa mbunge jimbo la Bunda Mjini Mhe Robrt Chacha maboto.
Na Adelinus Banenwa
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Mhe Robert Chacha Maboto amesema kuanzia Juni 16, 2024 atawakatia bima za afya wazee wapatao 198 kutoka jimbo la Bunda mjini na kuwafungulia ofisi yao itakayoweza kuwasaidia kujadili mambo yao hapo.
Mhe Maboto ameyasema hayo katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee iliyofanyika leo Juni 15, 2024 ambayo yamefanyika mjini Bunda katika viwanja vya shule ya msingi miembeni.
Mhe Robert Chacha Maboto amesema katika maisha yake tangu alipojitambua amekuwa na utaratibu wa kuwathamini wazee na hii ni kulingana na vitabu vya dini visemavyo kuwa muheshimu baba na mama yako upate kuishi miaka mingi na yenye kheri duniani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wa baraza la ushauri la wazee Tanzania ndugu David Lameck Sendo amesema kupitia maadhimisho hayo, baraza la wazee Tanzania wanatoa tamko ambalo ni Kukemea mauaji, unyanyasaji na ukatili wowote ule dhidi ya wazee na makundi maalumu mengine wakewemo wanawake na watoto, Uwekezaji kwa watoto wa kike na wanawake ni mwiko, Ushoga Tanzania ni mwiko, Aidha mwenyekiti Sendo amesema pia ni baraza la ushauri la wazee Linakemea vyombo vya habari mtandaoni kuacha kurusha maudhui yasiyofaa.
Naye Kanal Evance Mtambi mkuu wa mkoa wa Mara kwa niaba ya waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Dk Doroth Gwajima amesema amewataka wazee kuwa chachu ya malezi kwenye jamii, na kuacha kushiriki kwenye mila potofu hasa za ukeketaji na kulazimisha kuoza wajane.
Aidha amewataka vijana kutunza wazee wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu ili kama vile matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuwaokoa na tatizo la ugonjwa wa macho.