Marufuku kuharibu picha za wagombea kipindi cha kampeni uchaguzi mdogo Mara
8 March 2024, 4:58 pm
Ubanduaji,kuchana picha za wagombea ni marufuku kipindi cha kampeni uchaguzi mdogo Mara
Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imekemea vitendo vya ubanduaji au kuchana picha za wagombea au kubandika picha ya mgombe juu ya picha ya mgombea mwingine wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani.
Na Adelinus Banenwa

Hayo yamesemwa na afisa wa tume ya taifa ya uchaguzi Bi Maria Petro Dadu wakati akifanya mazungumzo na radio mazingira fm kuhusu kampeni zinazoendelea kuelekea uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika March 20, 2024.
Bi Maria amesema kwa mkoa wa Mara kata mbili zinashiriki katika uchaguzi huu mdogo wa udiwani, kata hizo ni Busegwe kutoka wilaya ya Butiama na kata ya Mshikamano kutoka wilaya ya Musoma.