Madiwani Bunda walia na uvamizi wa nyani kwenye makazi
17 February 2024, 10:25 pm
Tutazungumza na tawa kutatua changamoto ya uvamizi wa nyani kwenye makzi ya watu Mhe Madiwani tupeni muda.
Na Adelinus Banenwa
Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda kupitia kwa katibu tawala wilaya hiyo Salumu Mtelela imelihakikishia baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Bunda kuwa ofisi hiyo itakutana na mamlaka zinazohusika katika usimamizi wa wanyamapori ili kutatua changamoto ya uvamizi wa nyani na nguruwepori katika makazi ya watu.
Ni katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Bunda cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023 na 2024 kilichoketi Feb 14 , 2024.
Kauli hiyo ya Mtelela imekuja baada ya diwani wa kata ya Kabarimu Ndugu Muhunda Nyahimbo Manyonyoryo kutaka kujua hali ya nyani na nguruwepori kufanya uvamizi kwenye makazi ya watu pamoja na mashamba ambayo yameshuhudiwa katika siku za hivi karibuni hasa katika maeneo ya kata ya Kabarimu mtaa wa Saranga na Kilima hewa, kata ya Nyamakokoto, Balili miongoni mwa maeneo mengine.
Katika hoja zao madiwani wamedai kuwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bunda na Hospitali ya Bunda DDH yamekuwa kitovu cha uvamizi wa nyani na imekuwa ni usumbufu kwa wagonjwa hasa akina mama waliojifungua kuwa kwenye hatari ya kunyang’anywa vyakula vyao.