Upatikanaji wa maji Bunda kufikia 92% mwaka huu
16 January 2024, 12:43 pm
Mamlaka ya maji Bunda BUWASSA imesema miradi yote ya maji inayotekelezwa mjini Bunda ikikamilika itafanya upatikanaji wa maji mjini Bunda kufikia asilimia 92.
Na Adelinus Banenwa
Mamlaka ya maji Bunda BUWASSA imesema miradi yote ya maji inayotekelezwa mjini Bunda ikikamilika itafanya upatikanaji wa maji mjini Bunda kufikia asilimia 92.
Hayo yamesema na Eng Jumanne Seleli Meneja wa usambazaji maji kutoka BUWASSA walipotembelea mradi wa Mugaja – Manyamanyama ambao unagharimu fedha za kitanzani zaidi ya shilingi billion 1,1 ambapo ujenzi wake umeanza tangu mwezi October mwaka jana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa BUWASSA Bi Ester Giryoma amesema anaipongeza serikali kwa kuwapatia fedha nyingi katika usambazaji maji na hawana shaka kama BUWASSA kufikia adhma ya serikali ya asilimia 95 ya upatikanaji wa maji ifikapo 2025.
Aidha amesema kwa Bunda hakuna changamoto ya mgao wa maji ila changamoto ipo pale umeme unapokatika huku akiwatoa hofu wananchi juu ya gharama ya huduma ya maji kwa unit akibainisha ni kutokana na maelekezo ya EWURA wanaopanga bei.