RC Mtanda awataka Nyatwali kuendelea na shughuli zao
8 January 2024, 7:23 am
Mkuu wa mkoa wa mara Mhe Said Mohamed Mtanda amewataka wakazi wa Nyatwali kuendelea na shughuli zao za kawaidi huku serikali ikiendelea kufanya ufuatiliaji wa wao kuhama.
Na Adelinus anenwa
Mkuu wa mkoa wa mara Mhe Said Mohamed Mtanda amewataka wakazi wa Nyatwali kuendelea na shughuli zao za kawaidi huku serikali ikiendelea kufanya ufuatiliaji wa wao kuhama
Mhe Mtanda ameyasema hayo leo katika ziara yake wilayani Bunda ambapo pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali pia amefanya mkutano wa hadhara na wakazi wa kata ya Nyatwali ambao wapo katika mchakato wa kuamishwa
Mhe Mtanda amesema serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha kila mwananchi wa Nyatwali anapata haki yake inayostahili hivyo kwa kipindi hiki ambacho serikli bado inaendelea na utaratibu wake wananchi wa Nyatwali waendelee na shughuli zao pia wanafunzi wanatakiwa kupelekwa shule.
Mheshimiwa Mtanda amesema zoezi la uthamini lilishakamilika na kupelekwa kwa mthamini Mkuu wa Serikali ambapo imebainika kuwa jumla ya shilingi Bilioni 59 zinahitajika kulipa fidia kwa wananchi 4111 waliofanyiwa uthamini na kujaza fomu namba 69 ambayo ni fomu ya kukubali kufanyiwa uthamini.
Kauli hiyo ya mkuu wa mkoa imekuja baada ya Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto aliyetaka kujua hatma ya wakazi wa Nyatwali kutokana na kukaa muda mrefu bila kulipwa fedha zao wakati tayari wamekwisha fanyiwa tathmini ya mali zao.
Kwa upande wao wakazi wa Nyatwali kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya wananchi wa nyatwali wamesema mambo manne ambayo yanachangamoto katika mchakato wa kuamishwa kwao ni pamoja na kuonekana analipwa nauli mtu mmoja kwenye familia, mifugo na mitumbwi kutofanyiwa miongoni mwa changamoto zingine.