Maryprisca: Vitongoji vyote Tiring’ati kupata maji ya ziwa Victoria
12 December 2023, 4:43 pm
Naibu Waziri wa Maji Mhe Maryprisca Mahundi amefanya ziara katika jimbo la Bunda huku akiahidi vitongoji vyote vya kijiji vha Tiring’ati kupatiwa huduma ya maji.
Na Adelinus Banenwa
Naibu Waziri wa Maji Mhe Maryprisca Mahundi amefanya ziara katika jimbo la Bunda huku akiahidi vitongoji vyote vya kijiji cha Tiring’ati, shule ya sekondari Esperanto na shule ya msingi Kambarage kupata maji safi na salama haraka.
Mhe, Mahundi ameyasema hayo katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara iliyoanza leo katika jimbo la Bunda ambapo amesema serikali katika kuhakikisha changamoto ya maji inaisha katika maeneo ya Nyamuswa na viunga vyake serikali inakwenda kuunganisha maji ya mradi wa Mgango Kyabakari ambapo mabomba yakuleta maji katika mji wa Nyamuswa yatatokea Butiama na litakuwa na urefu wa kilometer 18
Aidha amewaelekeza RUWASA mkoa kubadilisha mtandao wa mabomba chakavu na kuweka mabomba yanayoendana na idadi ya watu waiopo Kwa Sasa.
Kwa upande mwingine Mhe Mahundi amekitaka chombo Cha watumia maji kufanya marekebisho ya changamoto ndogo ndogo ili miradi izidi kuwepo huku akiwataka wananchi kuchangia Ankara za maji
Mhe, Mahundi pia amewataka wananchi kuacha kuhujumu miundombinu ya maji kama vile kuweka mawe kwenye visima vya maji.
Kauli hiyo ya Mhe naibu waziri imekuja kufaitia maombi ya Mhe diwani wa kata ya Ketare Mramba Simba Nyamkinda na mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphasi Mwita Getere mbele ya mhe naibu waziri wakimtaka awasaidie kutatua changamoto ya maji katika maeneo yao kwa kuwaunganisha na mradi wa Mugango Kyabari.