Keraryo aikumbuka shule aliyosoma, atoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni sita
14 October 2023, 7:26 pm
Vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi milioni 6 vimetolewa shule ya msingi Nyerere iliyopo kata ya Balili halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara na mwanafunzi aliyehitimu shuleni hapo Joseph Kiraryo.
Na Adelinus Banenwa
Vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi milioni 6 vimetolewa shule ya msingi Nyerere iliyopo kata ya Balili halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara na mwanafunzi aliyehitimu shuleni hapo Joseph Kiraryo.
Akizungumza katika kupokea vifaa hivyo mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Anney amesema ni watu wachache sana wenye moyo kama wa Joseph wa kukumbuka alikotoka hasa shuleni na kusaidia mahitaji.
Kwa upande wake Joseph kiraryo ambaye ni mwanafunzi aliyehitimu shuleni hapo mwaka 2011 amesema baada ya kufika shuleni hapo na kugundua kuna changamoto nyingi aliahidi kusaidia kadri mungu atakavyo muwezesha
Aidha vifaa alivyo kabidhi leo ni pamoja na mashine ya kurudufu karatasi photocopy mashine komputa moja na karatasi za kuchapia mitihani limu paper 20 vyenye thamani ya shilling million 6
Mwalimu mkuu shule ya msingi nyerer mwalimu Edwin Johakim Byangwamu amemshukuru kijana huyo kwa kuweza kuwasaidia vifaa hivyo ambapo amesema awali walikuwa wakitumia gharama kubwa katika kuchapisha mitihani au wakati mwingine walimu kulazimika kuandika maswali yasiyopungua 45 ubaoni jambo lililokuwa likiwachosha walimu hao
Byangwamu ameiambia mazingira fm kwamba tangu afike shuleni hapo amekuwa na utamaduni wa kuwatafuta wadau kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo huku akitaja kuwa wakati anahamia shule hiyo alikuta zaidi ya wafunzi mia tatu (300) wanakaa chini lakini kupitia wadau hadi kufikia siku ya leo wanafunzi wote wanakaa kwenye dawati