Majukwaa ya wakulima chachu Kwa wakulima wadogo
20 September 2023, 10:06 am
Kilimo kimeendelea kuwa muhimu katika kuchangia Pato la taifa (GDP) na uchumi wa nchi.
Na Thomas Maswali
Kilimo kimeendelea kuwa muhimu katika kuchangia Pato la taifa (GDP) na uchumi wa nchi.
Katika mwaka 2019 mchango wa kilimo katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 26.9 na kwa mwaka 2020 sekta ya kilimo imekua kwa asilimia 4.9 ilinganishwa na asilimia 4.4 ya mwaka 2019.
Maendeleo ya kilimo yamekuwa chini ya serikali kwa kipindi kirefu lakini marekebisho ya uchumi yamekuwa yakiendelea kuwa na matokeo muhimu kwenye sekta ya kilimo.
Aidha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wamekua na mawazo mbalimbali ya kuwakwamua wakulima kama ambavyo shirika la Vi Agroforestry kwa ushirikiano na shirika la Civic social protection (CSP) ambavyo wamekuja na mradi wa ASILI-B wenye malengo ya kuimarisha kilimo kuwa kilimo endelevu na chenye tija, kuimarisha taasisi za wakulima na usalama wa chakula wenye kuchochea lishe bora.
Katika kuhakikisha hilo linatekekezeka wameanzishaji wa majukwaa ya kilimo nchini, ambayo yanatajwa kuwa chachu kwa wakulima katika kufanya uchechemuzi wa masuala ya sheria, kisera, miongozo na taratibu katika kilimo chenye tija.
Uwepo wa majukwaa ya kilimo kutasaidia kubeba ajenda mbalimbali za wakulima katika kilimo endelevu chenye kuboresha Maisha, kuimarisha taasisi za kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo yamesemwa leo na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Civic social protection foundation (CSP) bwana Nemes Elia wakati akifanya mazungumzo na radio Mazingira fm katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Butiama kuhusu uanzishwaji wa majukwaa hayo.
Bwana Elia amesema hadi sasa wamefikia mikoa mitatu ambayo ni Mara, Kagera na Dodoma lengo ni kuona majukwaa imara ambayo yataweza kubeba ajenda na kuona wakulima wadogo wakishirikishwa kwenye bajeti za halmashauri pamoja na kuwaongezea uwezo wakulima waweze kupasa sauti kupitia majukwaa hayo.
Bwana Elia amesema hayo yote yanatekelezwa kupitia mradi wa ASILI-B unaotekelezwa na shirika la Vi Agroforestry kwa ushirikiano na shirika la Civic social protection( CSP) wenye lengo la kuimarisha kilimo endelevu na stahamilivu wenye kuboresha Maisha ya wakulima.