Dr. Lawrence Mbwambo aifafanua WWF kwa Naibu Waziri wa Maji
17 September 2023, 11:54 am
Na Edward Lucas
“Ni shirika ambalo lipo Tanzania tangu miaka ya 1960 likifanya kazi hasa za Uhifadhi wa Wanyamapori lakini miaka ya 1990 liliongeza uwanda wa Uhifadhi na kuongeza programu za misitu, maji baridi, mazao ya bahari na nishati ” Dr Lawrence
Hayo yamesemwa na Meneja wa Uhifadhi wa WWF Tanzania, Mhandisi Dr. Lawrence Mbwambo kupitia maadhimisho ya Mto Mara katika viwanja vya Sokoine mjini Mugumu wakati walipotembelewa katika banda lao na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Dr Lawrence amesema WWF ipo mkoa wa Mara kwa takribani miaka 20 ikiangalia zaidi chanzo Cha maji dakio la maji Mto Mara.
Kwa upande wake, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapongeza WWF Tanzania na kueleza kuwa shughuli zao wanazitambua na kwamba wamekuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi za serikali.
Katika Maadhimisho hayo ambayo ni ya 12 tangu kuasisiwa kwake mwaka 2012, WWF Tanzania wametunukiwa tuzo mbili ambazo ni “Mara River Conservation Champion (Mabingwa wa Uhifadhi Mto Mara)” na “Best Exhibitor (Muoneshaji Bora)”