Wakulima watakiwa kulima kilimo hifadhi kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi
14 September 2023, 7:49 pm
Wito umetolewa kwa wakulimakutumia teknolojia ya kilimo hifadhi ili kupata mazao mengi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea kushuhudiwa duniani kwa sasa.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wakulimakutumia teknolojia ya kilimo hifadhi ili kupata mazao mengi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea kushuhudiwa duniani kwa sasa
Wito huo umetolewa na Shija Lucas ambaye ni msimamizi wa mpango huo kutoka kanisa la AICT MARA ambapo lengo la mpango huo ni kuwasaidia wakulima kubadili namna ya kulima ikiwa ni pamoja na njia za urutubishaji udongo katika mashamba yao.
Aidha Ndugu Shija ameeleza kuwa tangu kuanza kwa mpoango huo kumewasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima ambapo sehemu ambayo mkulima alikuwa akipata gunia mbili kabla ya kupata elimu ya kilimo hifadhi sasa hivi anapata hadi gunia 10 na kuendelea katika shamba hilohilo.
Kwa upande wao wakulima kutoka kijiji cha Kyabakari wilayani Butiama wamesema wanayaona mabadiliko makubwa tamgu waanze kutumia teknolojia ya kilimo hifadhi ukilinganisha na mwanzo hasa katika upande wa mavuno kwenye zao la mahindi.