Mazingira FM

Bunda, Mchungaji Motomoto Atoa vifaa vya shule kwa wanafunzi 275 wa Awali Msingi na Sekondari

1 January 2023, 7:16 pm

Jumla ya madaftari 806, kalamu 150 na box mbili za pensel vimetolewa kwa wanafunzi 275 wa ngazi tofauti wanaotalajiwa kuanza muhula wa masomo hivi karibuni

 

Vifaa hivyo vya shule vimetolewa na mchungaji kiongonzi wa kanisa la Revival Buptst Nyasura JEREMIA MOTOMOTO ambapo amesema vifaa hivyo vimewalenga watoto ambao ni wahitaji na ni moja ya kazi wanazofanya za kuwajengea watoto fikra ya utoaji na anaamini vifaa hivyo vitawasaidia katika masomo yao

 

Wanafunzi walionufaika na vifaa hivyo ni wanafunzi 200 kutoka shule za msingi ambao wamepata jumla  daftari 600 wanafunzi wa asekondari 30 wakipata jumla daftari kubwa 86 na wanafunzi wa awali 45 wakipata jumla daftari 120 .

Aidha amewaasa wanajamii kwa ujumla kuweze kushiriki katika kuwasaidia waitaji amboa wapo kwenye jamii.

Kwa upande wao watoto ambao wamepokea sehemu ya vifaa hivyo wamemshukuru Mchungaji motomoto na kanisa la Baptist kwa ujumla juu ya moyo wa upendo waliounesha kwa kuwapatia vifaa hivyo.