Mazingira FM
Mazingira FM
22 January 2026, 8:01 am

Tangu waanzishe program hiyo imeweza kusaidia jumla ya wanafunzi 15668 na wanajamii 6880
Na Mariam Mramba
Jumla ya wanafunzi 254 kutoka shule za msingi na sekondari wanaotoka mazingira magumu wamepokea msaada wa vifaa na mahitaji malimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni sabini na nane kutoka shirika la project zawadi.
Akisoma taarifa ya shirika hii leo January 19 2026 katika hafla ya ugawaji vifaa kwa wanafunzi iliyofanyika Nyamuswa Meneja wa mradi wa mafunzo ya walimu bwana Nehemia Kipande amesema kuwa tangu waanzishe program hiyo imeweza kusaidia jumla ya wanafunzi 15668 na wanajamii 6880 ambapo pia wamefanikiwa kuborsha miundo mbinu mbalimbali ikiwemo kujenga madarasa ,nyumba za walimu, kukarabati madarasa, zaidi ya madawati 600 yametengenezwa na kujenga miradi ya maji.
Baadhi ya wazazi ambao Watoto wawamenufaika na msaada huo wamesema licha ya Watoto wao kupata mahitaji yote bado miomgoni mwao wamekuwa hawahudurii masomo ipasavyo ambapo awetoa wito kwa wazazi kuhakikisha Watoto wote wanao pata mahitaji wanazingatia masomo na kwamba wazazi ambao wanachangia utoro kwa wanafunzi wachukuliwe hatua za kisheria.
Kwa niaba ya Meneja mkazi wa shirika hilo Bi Rejina amesema kuwa amesema kuwa hayo yote yanayofanywa na shirika hilo ni kuwa nania njema ya kutaka vijana wa kitanzania kupata elimu bora kuwaomba wanafunzi, wazazi,walimu serikali paamoja na shirika hilo kushirikiana kwa Pamoja ili kupiga hatua katika sekta ya elimu.
Mkuu wa wilaya ya Bunda Aswege Enock Kaminyoge ambaye alikuwa mgeni rasimi katika hafla hi awetoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha Watoto wote ambao wanatakiwa Kwenda shule wafike shuleni kama walivyoelekeza kwani hadi sasa idadi ya wanafunzi waliokwisha ripoti shuleni hairidhishi ambapo pia ametumia furusa hiyo kuwapongeza Sshirika la project za Wadi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusaidia Watoto katika kupata elimu bora.