Mazingira FM

Maboto apokea hati ya pongezi kutoka TRA

23 December 2025, 4:10 pm

Josephine wamepokea kwa moyo wa shukrani hati hiyo na imekuwa ni desturi yao kuhakikisha wanalipa kodi vizuri.

Na Adelinus Banenwa

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mara wamekabidhi hati ya pongezi kwa Maboto Microfinence kwa kuwa mlipakodi bora kwa mwaka 2025

Akikabidhi hati hiyo ya pongezi meneja wa TRA Mkoa wa Mara amesema wameamua kutoa hati hiyo ya pongezi kutokana na ulipaji wao wa kodi usiyo na mashaka wala wa shuruti huku akibainisha kuwa si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kufanya vizuri katika ulipaji wa kodi.

Kwa upande wake Josephine Gerald ambaye ni muhasibu wa Maboto Microfince tawi la Bunda kwa niaba ya mkurugenzi Robert Chacha Maboto amesema wamepokea kwa moyo wa shukrani hati hiyo na imekuwa ni desturi yao kuhakikisha wanalipa kodi vizuri.

Sauti ya Josephine Gerald

Amesema katika kipindi hiki kuelekea kufunga mwaka taasisi hiyo imepata changamoto kutokana na madhira ya wakati wa uchaguzi ambapo makao makuu yao yalichomwa moto hali iliyopelekea nyaraka na rasilimali nyingi kuteketea na baadhi ya wafanyakazi kusimamishwa kutokana na hasara hiyo.

Sauti ya Josephine Gerald