Mazingira FM
Mazingira FM
7 December 2025, 12:45 pm

Mhe Aswege Enock Kaminyoge ameitaka halmashauri kuandaa mafunzo kwa madiwani hao ili kuwakumbusha majukumu yao kwa mujibu wa miongozo sheria na kanuni za kudumu za halmashauri.
Na Adelinus Banenwa
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda limemchagua Mhe Renatus Mujungu Mujungu kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kura 26 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa

Pia baraza hilo limemchagua Mhe Kiremba Irobi kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kupata kura 26 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa.
uchaguzi huu umefanyika Dec 5, 2025 katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Katika ujumbe wa mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Aswege Enock Kaminyoge katika baraza hilo la madiwani baada ya kuapishwa ameitaka halmashauri kuandaa mafunzo kwa madiwani hao ili kuwakumbusha majukumu yao kwa mujibu wa miongozo sheria na kanuni za kudumu za halmashauri.
Kingine Mhe DC ameelekeza uwepo ushirikiano baina ya madiwani na wataalamu wa halmashauri ili kusimamia vyema shughuli za maendeleo za halmashauri hiyo.
Akigusia vurugu za wakati na baada ya uchaguzi Mhe Aswege amesema vurugu hizo huenda ni matokea ya wananchi kukosa majibu kutoka kwa viongozi wa serikali hivyo ameagiza kuhakikisha viongozi wanatoa majibu sahihi kwa wananchi ili kuondoa maswali na malalamiko miongoni mwao

Akihailisha kikao cha kwanza cha baraza hilo mwenyekiti wa halmashauri hiyo Renatus Mujungu Mujungu amesema ushirikiano baina ya waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo ndiyo utakuwa msingi wa maendeleo ya halmashauri.
Katika baraza hilo jumla ya madiwani 26 wameapishwa wakiwemo 19 kutoka kata za halmashauri hiyo na madiwa 7 wa viti maalumu