Mazingira FM
Mazingira FM
20 November 2025, 7:55 pm

Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa UVIDA una athari nyingi ambapo ni pamoja na gharama kubwa ya matibabu, hatari ya ugonjwa wa figo n.k
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa jamii kuhakikisha wanamaliza dozi za dawa wanazokuwa wamepewa na watoa huduma za afya pindi wanapokuwa wanaumwa.
Hayo yamesemwa na Frank Gasper Muhini, Afisa wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya ziwa mashariki wakati alipokuwa akitoa semina kwa wanafunzi wa chuo cha ualimu Bunda ambapo amesema ni vema mtu anapopewa dawa kutumia na mtoa huduma wa afya ahakikishe anaimaliza.

Frank ameongeza kuwa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa UVIDA una athari nyingi ambapo ni pamoja na gharama kubwa ya matibabu, hatari ya ugonjwa wa figo miongoni mwa hatari zingine.
kwa upande wao wanafunzi wameishukuru mamlaka kwa kutoa semina na elimu kwao juu ya matumizi sahihi ya dawa hali inayoweza kusaidia kupunguza hari zinazoweza kujitokeza kutokana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.