Mazingira FM
Mazingira FM
25 October 2025, 8:40 pm

Asema endapo atachaguliwa, kipaumbele chake kitakuwa ni kuinua maendeleo ya wananchi wa Bunda Mjini
Na Thomas Masalu
Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Bunda Mjini, Estar Bulaya, amehitimisha kampeni zake leo katika viwanja vya Stendi ya Zamani vilivyopo katikati ya mji wa Bunda mkoani Mara.
Katika hotuba yake ya kufunga kampeni, Bi. Bulaya amewashukuru wananchi wa Bunda Mjini kwa ushirikiano waliompa kipindi chote cha kampeni na kuwaomba kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wao ili aweze kutekeleza kwa vitendo ahadi alizotoa.

Ameeleza kuwa endapo atachaguliwa, kipaumbele chake kitakuwa ni kuinua maendeleo ya wananchi wa Bunda Mjini akitanabaisha kuwa changamoto kubwa ya wilaya ya bunda ni tatizo la miundombinu ya barabara ambapo amehaidi kushirikiana ana TARURA na TANROAD kuweka miundombinu vizuri

Pia ametaja suala la kusimamia huduma bora za afya , mikopo ya asilimia kumi ya vikundi miongoni mwa ahadi zingine
Aidha , Bulaya amesema ataenda kuhakikisha mradi wa ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa unatekelezwa, itakayoweka hadhi ya mji wa Bunda na kuchochea maendeleo ya biashara.