Mazingira FM
Mazingira FM
18 October 2025, 8:23 pm

“TAKUKURU hatutasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo la kisheria“
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa kufanya sherehe baada ya kushinda uchaguzi na kualika watu unaodhani wamekupigia kura ili ushinde ni rushwa.
Hayo yamesema na William Eliyau Afisa uchunguzi kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilaya ya Bunda wakati akizungumza na wananchi kupitia mazingira fm kwenye kipindi cha ufahamu wa sheria.

Eliyau amesema sherehe pekee kwa aliyeshinda anayotakiwa kuifanya ni kutekeleza ahadi alizoahidi kwa wananchi na si kuandaa vyakula wala fedha wala vinywaji.
Amesema TAKUKURU hawatasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo la kisheria