Mazingira FM
Mazingira FM
11 October 2025, 6:19 pm

Miongoni mwa mazao yanayoweza kulimwa kuwa ni pamoja na mahindi, mpunga, alizeti mbogamboga ambapo viwanda vya kuchakata mazao hayo vitapatikana hapo pia.
Na Adelinus Banenwa
Malongo Mashimo aliyekuwa diwani kata ya Nyatwali 2020 na 2025 ameishauri serikali kulifanya eneo la EPZ Bunda kuwa eneo la shughuli za kilimo cha umwagiliaji na uongezaji thamani bidhaa mbalimbali ili kuwakwamua vijana kiuchumi.
Malongo ameyasema hayo leo katika mahojiano na radio mazingira fm ambapo amesema kupitia kitabu kidogo cha ilani ya chama cha mapinduzi cha mkoa wa Mara ameona kumeandikwa fursa za kilimo hivyo kwa Bunda endapo eneo la EPZ likitumika katika kilimo cha umwagiliaji katika mazao mbalimbali na kuanzishwa viwanda vya uchakataji mazao litaleta tija kubwa kwa vijana wasiyokuwa na ajira.
Ametaja miongoni mwa mazao yanayoweza kulimwa kuwa ni pamoja na mahindi, mpunga, alizeti mbogamboga ambapo viwanda vya kuchakata mazao hayo vitapatikana hapo pia maduka ya pembejeo yatapatikana hapo na kisha serikali itawaunganisha na masoko jambo litakalosaidia sana vijana
Aidha amewashauri vijana kuacha tabia ya kutaka mafanikio ya haraka na badala yake wajenge tabia ya kujiamini na kukua kwa hatua na kutafuta kwanza ujuzi katika fani mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali zikiwemo veta na mashirika binafsi