Mazingira FM
Mazingira FM
30 September 2025, 6:59 pm

Watu watano wamenusurika kifo baada ya tembo kushambulia nyumba waliyokuwemo.
Na Adelinus Banenwa
Ni katika mtaa wa Tairo uliopo kata ya Guta halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara ambapo nyumba ya mzee Juma Sarya kushambuliwa na tembo ikiezua mabati na kuangusha kuta za nyumba hiyo.
Manusura wa tukio hilo wameiambia Mazingira Fm ilipofika eneo la tukio wamesema ilikuwa majira ya saa moja asubuhi tarehe 27 Sept 2025 ambapo kundi la tembo kama 30 walionekana wakitoka maeneo ya Kinyambwiga kuelekea hifadhini.
Manusura hao wamesema kutokana na tembo hao kuwa wengi iliwabidi wakimbie kuingia ndani ya nyumba na baada ya kundi hilo kupita walitoka nje kisha wakaona tembo wengine watatu ambao hao ndiyo waliofanya uharibifu katika moja ya nyumba ya mzee Sarya.
Juma Sarya baba wa familia amesema tukio hilo la tembo kufanya uharibifu wa nyumba yake umeleta adha kubwa kwake ambapo baada ya tukio maliasili walifika kwake na kumtaka ajaze fomu kisha aipeleke maliasili kwa ajili ya utaratibu mwingine kuendelea.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa tairo George Joshua Daud amesema ni kweli alipokea taarifa za tukio hilo na alifika na Maafisa wa maliasili na walimshauri kujaza fomu kwa ajili ya utaratibu mwingine.
George amesema adha ya tembo imeongezeka tangu wananchi wa Nyatwali kuhamishwa ambapo kwa sasa makundi ya tembo yamekuwa makubwa katika eneo hilo la tairo