Mazingira FM
Mazingira FM
26 September 2025, 7:00 pm

Kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1278 ambapo kati yao wavulana ni 616 na wasichana ni 662.
Na Adelinus Banenwa
Upungufu wa walimu wa sayansi na Sanaa, ukosefu umeme kwenye madarasa, ukosefu wa jiko, upungufu wa matundu ya Vyoo, ukosefu wa nyumba za walimu pamoja ukosefu wa vifaa vya tehama bado ni changamoto katika maendeleo ya taaluma shule ya sekondari ya Migungani.

Hayo yamesema na mkuu wa shule ya sekondari ya Migungani Mwl Boaz Tekere kupitia taarifa ya katika mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika leo tarehe 25 Sept 2025 ambapo amesema kuwa kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1278 ambapo kati yao wavulana ni 616 na wasichana ni 662.

Mwl Boaz amesema kwa sasa shule hiyo inapitia hasa changamoto ya hasa ya ukosefu wa umeme madarasani unawanyima fursa wanafunzi kujisomea wakati wa jioni na ukosefu jiko unapelekea kuwepo na adha hasa kipindi cha mvua wakati wa maandalizi ya chakula cha wanafunzi.